Indirimbo ya 73 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Najua njia moja yakufika mbinguni, ingawa ikipita katika majaribu, lakini iendako mjini huko juu,:/: Na njia hiyo Yesu.:/:
2
Najua na amani iliyo ya milele, huwezi kuipewa kwa fedha na dhahabu; ni tunu ya rehema iliyotoka Baba.:/: Amani hiyo Yesu.:/:
3
Najua nguvu moja yakuniponya roho, initiayo raha, amani na faraja, inanilinda vema na nguo yangu safi,:/: Na nguvu hiyo Yesu:/:
4
Najua na kifiko mbinguni huko juu, na siku ni karibu kita’poonekana. Yafa’kukaza mwendo, kupiga mbio sana!:/: Kifiko ni mbinguni.:/: