Indirimbo ya 11 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Ikiwa wananiuliza msingi wa uzima, Je, twahitaji kuongeza kwa kazi yake Yesu? Kwa uhodari nitajibu: Msingi wangu ni wa nguvu, ni damu yake Yesu Kristo, inanitosha sana.
2
U mwamba wa zamani sana, daima utadumu. Na hata siku nitakufa, nitautegemea. Nitakapoondoka huku, nitamsifu mwana kondoo, na damu ya Mwokozi wangu, funguo la mbinguni.