Indirimbo ya 117 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Nilipofika Golgotha nikaiona huko neema kubwa kama mto, neema ya ajabu.
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne’ma tele na ya milele, ne’ma ya kutosha!
2
Nilipofika moyo wangu ulilemewa sana, sikufaamu bado vema neema yake kubwa.
3
Nilipoona kwamba Yesu alichukua dhambi, neema ikadhihirika, na moyo ukapona.
4
Mbinguni nitakapofika, furaha itakuwa kuimba juu ya neema milele na milele.