Indirimbo ya 120 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Msalabani nilimwona Yesu, Mwokozi wangu aliyeniponya; rohoni mwangu giza ikatoka, ninafuata Yesu sasa.
Nimeokoka kutoka dhambi, na siku zote ninaimba kwa furaha. Ni vita kali kushinda yote, lakini Yesu yu karibu.
2
Mwokozi wangu ananipa nguvu, nikiuona udhaifu huku. Na vita yote itakapokwisha, nitaipata raha kwake.
3
Mwokozi wangu, ninakufuata, furaha yako inanituliza. Na siku moja utakuja tena kunichukua huko kwako.