Indirimbo ya 123 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Mwokozi mzuri ninaye, zamani sikumfahamu, na sasa ninamhubiri, wengine wapate kuona.
Wote watamwona, wote watamwona Mwokozi mzuri ninaye; Lo! Wote watamwona.
2
Shetani akinizuia nisimfuate Mwokozi, najua Bwanangu hodari hutaka kunisaidia.
3
Apita wo wote kwa wema, mfano ‘tukufu wa Baba, lakini anitaja ndugu, niliye maskini kabisa.
4
Natoa maisha na pendo kwa Yesu aliyenipenda. Katika ishara za Mungu upendo wapita yo yote.