Indirimbo ya 132 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yesu Mwokozi, unanipenda, na pendo lako ni kubwa kabisa. Ulinivuta karibu nawa, Mimi ni wako daima dawamu.
2
Yesu Mwokozi, unanipenda, na pendo lako lapita akili. Linanifunza kuzifahamu raha, upole na utu adili.
3
Yesu Mwokozi, unanipenda, mimi maskini, dhaifu, mnyonge. Nimetakaswa kwa damu yako; ninakuomba, ‘nijaze upendo!
4
Yesu Mwokozi, unanipenda, umenitilia wimbo kinywani wa kukusifu hata milele, nitakuona halisi mbinguni.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 132 mu Nyimbo za wokovu