Indirimbo ya 133 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Ufurahi, moyo wangu, heri nyingi umepata!
:/: Sikitiko limekwisha, Yesu ni wangu nami wake.:/:

2
Ameponya roho yangu, yeye ni mponyaji mwema;
:/: Na kwa Roho ‘takatifu anabatiza watu wake.:/:

3
Jina langu ni mbinguni, Yesu ameliandika.
:/: Mimi mali ya Mwokozi hata milele na milele.:/:

4
Na moyoni mwangu sasa ninaimba: Mungu, Baba!
:/:Ni furaha kubwa sana, nina rafiki kila saa.:/:

5
Nimeondolewa dhambi, nisitende ovu tena!
:/: Kwani Yesu aokoa kila wakati na dakita.:/:

6
Nyimbo za kusifu Mungu zinajaa mbingu zote.
:/: Moyo wangu unajibu: Amina. Mungu asifiwe»:/: