Indirimbo ya 14 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Mwokozi wangu ulikwenda juu kukaa kuumeni kwake Baba; Utakusanya sisi sote huko, mbinguni kwako, utatufikishsa.:/: Makao mema wa’tuandalia, unatungoja kwake Mungu Baba.:/:
2
Mwombezi wetu wewe, Yesu Kristo, kwa’jili yetu mbele yake Baba. Wachunga sana sisi, kundi lako, na watusaidia ‘jaribuni.:/: Na siku zote unatuombea, watushindia vita kali huku.:/:
3
Mikono yako uliwanyoshea walio wako, siku uli’kwenda; na hivyo siku utakaporudi utabariki wakuaminio.:/: Ulivyokwenda, utakavyorudi; niombe nikakeshe kwa imani!.:/: