Indirimbo ya 142 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Kwa namna nyingi nilitafuta kupata raha moyoni mwangu. Unyonge wangu haukukoma ila kwa Bwana Yesu.
2
Na moyo wenye hatia nyingi nilimwendea Mwokozi wangu, na alinipa wokovu wake na nguvu ya kushinda.
3
Kwa pendo kubwa Mwokozi wangu aliuweka uzima wake, si kitu mimi ulimwenguni, nina wokovu kwake.
4
Ijapo ninachukiwa huku ni mteule wa Bwana Yesu, napenda sasa kumfuata, nifike kwake Mungu!