Indirimbo ya 144 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Sawa na kisima safi, chenye maji mengi, mema, ni upendo wa Mwokozi ukaao ndani yake.
Yesu amelifungua lango zuri la mbinguni ili niingie humo kwa neema yake kuu.
2
Kama ndege awindavyo mara nyingi niliumwa, Moyo wangu ulilia, Yesu hakunifukuza.
3
Ni ajabu kubwa kweli, alinisamehe yote! Juu ya rehema yake ninaimba kwa furaha.
4
Asubuhi ya uzima nitafika mlangoni; kwa ajili ya upendo nitapata kuingia.