Indirimbo ya 153 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yesu Kristo alifufuka, akatoka kaburini. Furahini na msifuni, kwani alishinda kufa!
Habari njema: Alifufuka katika wafu! Yesu yu hai, naye atakuja tena.
2
Nguvu za mauti na dhambi Yesu Kristo alishinda; nasi sote tutashinda kwa nguvu yake ya ajabu.
3
Kundi dogo, msiogope, Bwana Yesu ni uzima! Aliziondoa dhambi na anawafariji moyo.
4
E’ wakristo, shangilieni, Yesu aliyefufuka yu karibu, atakuja na atatufufua sote!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 153 mu Nyimbo za wokovu