Indirimbo ya 155 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Katika matumaini kwa Mungu wangu nakaa katika raha na utulivu. Na yeye ni mwamba wangu, imara sana; katika dhoruba zote ananilinda.
2
Mwenyezi ni ngome yangu, sitatetema; siwezi kuhofu tena huzuni, shida. Ikiwa ni vita kali, sitaogopa; ni msaidizi wangu karibu nami.
3
Mahali pa kustarehe kwa Yesu Kristo; napata amani, raha, furaha kubwa. Faraja katika shida, gizani nuru, na katika pepo nyingi bandari nzuri.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 155 mu Nyimbo za wokovu