Indirimbo ya 165 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nitazamapo kwa imani Mwokozi wangu, nafurahi, naona utajiri wake anao Mungu, Baba yangu. Haleluya! Furaha kubwa, aniongoza siku zote! Nikiuona udhaifu, anichukuwa mikononi.
2
Sitasumbuka mimi tena, furaha inanijaliza; Na kwa upendo na rehema anisikia, nikiomba. Haleluya! Ananitunza, Ninastarehe kwa salama. Na ukitaka raha yake, mfungulie moyo wako!
3
Nilipokaa kati’ dhambi Nikaliona sikitiko, Lakini shaka na hukumu Zimeondoka kwangu sasa. Haleluya! Anipa nguvu Yakuyashinda majaribu. Rohoni mwangu nina raha, Nalindwa nayo siku zote.
4
Dhihaka na mateso yote si kitu kwangu kwa sababu nafarijiwa na Mwokozi, nakumbatiwa na babangu. Haleluya! Mwokozi wangu ananitunza kwa neema. Nikiwa na ‘dhaifu tena, natiwa nguvu kwa imani.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 165 mu Nyimbo za wokovu