Indirimbo ya 168 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nina ushirika na furaha kubwa, namtegemea Bwana Yesu. Wingi wa uheri kwa waaminio: Kustarehe mikononi mwake!
Raha, raha, raha kwa Yesu na amani! Raha, raha, nastarehe mikononi mwake.
2
Raha ya ajabu ni rohoni mwangu, namtegemea Bwana Yesu. Nuru huangaza njia niendayo; nastarehe mikononi mwake.
3
Woga na huzuni zinatoka kwangu, nikitegemea Bwana Yesu. Ninafarijiwa siku zote naye, nastarehe mikononi mwake.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 168 mu Nyimbo za wokovu