Indirimbo ya 175 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Shamba la Mungu limeiva, litayari sasa kuvunwa. Wavunaji mfike mbio kuyavuna mavuno yake!
Bwana Yesu, twakuomba, uwatume watenda kazi wakusanye miganda yote kwako Yesu, Mwokozi mwema!
2
Uwatume mapema sana, na wengine kati’ mchana, hata saa ya magharibi uwaite wavuni wako!
3
E’mkristo anakuita, wende mbio, usichelewe! Macho yako uyainue kwani Yesu aja upesi!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 175 mu Nyimbo za wokovu