Indirimbo ya 179 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Siku moja mavuno yataisha kabisa, baada ya hayo hukumu. Jua litazimika siku hiyo ya mwisho, na hutasikia injili.
Atakusanya ngano kwa furaha ghalani, bali makapi yote yatatupwa motoni. Rafiki, utakuwa wapi?
2
Mahubiri na nyimbo za wokovu wa Mungu zitakaponyamanza huku, uliyelikataa neno zuri la Mungu, utakaa wapi milele?
3
Watu wote wa Mungu wafikapo mbinguni kukaa pamoja na Yesu, wataimba kabisa kwa sauti ya nguvu kumshangilia Mwokozi.