Indirimbo ya 186 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Fanyia Mungu kazi, mbio usiku waja! Mtumikie Mungu siku zako zote! Anza mapema sana, dumu mchana kutwa! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.
2
Fanyia Mungu kazi kama kungali jua, usipoteze bure siku zako huku! Uyatimize yote bila kukosa neno! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.
3
Fanyia Mungu kazi, saa yapita mbio! Fanya bidii sana kuokoa ndugu! Mtumikie Mungu kwa nguvu yako yote! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.