Indirimbo ya 197 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Hapo nilipokuwa dhambini, niliumwa kwatika roho. Sasa ninafurahi kwa shangwe kwani Yesu ameniponya.
Ndiyo kazi kubwa ya ajabu: Mwokozi aliniokoa! Naye anapenda watu wote, atakuokoa wewe.
2
Dhambi zote nilizozitenda zimefutwa na Bwana Yesu. Sikitiko kwa ‘jili ya dhambi zilikoma nilipotubu.
3
Sasa mimi sitaki kurudi, nachukia kabisa dhambi. Nimeonja furaha ya Mungu na amani na raha yake.