Indirimbo ya 198 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ mtu mwenye kiu, ufike kwake Yesu,
:/: upate maji ya uzima, hutaona kiu kamwe!:/:
Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!
2
Na tazama, ndugu wengi wamekwisha kunywa!
:/: Ni heri kubwa, maji hayo hayatakauka kamwe!:/:
3
Na wewe unywe pia, upate nguvu sana!
:/: Tumia katika shindano upanga wa neno lake!:/:
4
Na mwendo wa imani uta’poumaliza,
:/: utayakunywa maji bora kwa Mungu mbinguni juu.:/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 198 mu Nyimbo za wokovu