Indirimbo ya 2 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Kijito kiko chenye damu itokayo Mwokozi. Kiwaoshacho wakosaji
:/: Na dhambi na uchafu.:/:
:/: Na dhambi na uchafu.:/:
2
Msalabani mnyang’anyi alikiona hima. Mnyonge mimi kama yeye
:/: Nitakasike pia.:/:
:/: Nitakasike pia.:/:
3
Mwokozi wetu, damu yako daima ina nguvu. Ya kuokoa wenye dhambi
:/: Wa makabila yote.:/:
:/: Wa makabila yote.:/:
4
Kijito hicho cha ajabu ni tumaini langu. Upendo wako nausifu,
:/: Nausifu hata kufa.:/:
:/: Nausifu hata kufa.:/:
5
Nimeamini, naamini uliye nifilia, Msalabani umetoa
:/: Maisha yako Yesu.:/:
:/: Maisha yako Yesu.:/: