Indirimbo ya 201 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Njoo, mwenye huzuni nyingi! Yesu anakungoja. Uje, atoe mzigo wako, ata’okoa wewe!
Njoo, uliye na huzuni! Njoo kwa Mungu wa neema! Roho wa Mungu anakuita, Yesu anakungoja.
2
Njoo, mwenye makosa mengi! Yesu anakungoja. Kwake neema na upendo tele! Ata’okoa wewe.
3
Njoo, leo uache dhambi! Yesu anakungoja. Ukilemewa moyoni mwako, uje kwa Yesu mbio!
4
Njoo, sasa, E’mwenye dhambi! Yesu anakungoja. Na ukitaka kumfuata, ata’okoa wewe.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 201 mu Nyimbo za wokovu