Indirimbo ya 228 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Wakati wa utoto wako, hujapoona shida bado, sauti ilikuambia: “Unipe sasa moyo wako!”
Wajua ni nani huyu anayekuita sasa? Ni Yesu, rafiki yako; anakuita: ” Njoo kwangu!”
2
Na katika ujana wako wausikia mwito wake, na jinsi utakavyoshinda shetani akikujaribu.
3
Wakati wa uzee wako dhambini ukiendelea hata kukaribia kufa, Mwokozi akuita tena.