Indirimbo ya 23 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Nikitazama kwa imani Mwokozi wangu, Yesu, nawaka kwa upendo wake, na ninavutwa kwake; naona majeraha yake, Mikono na ubavu wake, na humo najificha sana, moyoni mwa upendo.
2
Imanweli upendwaye, nilinde siku zote, mpaka nihamie kwako mbinguni mwa uheri! Milele na milele huko hakuna la kunizuia Nisimsifu Bwana Yesu kwa damu na jeraha.