1
Mikwaju itiapo giza na kivuli katika nchi ya Bersheba ya zamani, alitembea Ibrahimu asubuhi, na maumivu na huzuni ni rohoni, kwa kuwa aliitwa na Mwenyezi Mungu kutii amri yake bila nung’uniko. Na hapo akaomboleza: “E’ Bwanangu, wataka nitakutolea mwana wangu?”
2
Sauti ya Bwanake aliifaamu: “Mtwae sasa mwana wako wa pekee, ukamtoe mwana juu ya madh’bahu; kafara ya thamani ukanitolee!” Na moyo wake ukamtulia sana, akitukuza Mungu akitumaini yakuwa yeye atamfufua mwana; alimjuwa yeye aliye mwamini.
3
Akaamka Ibrahimu alfajiri, akatandika punda, akatwaa kuni. Pamoja na mwanawe tena ‘kasafiri, na roho yake ikalia kwa huzuni. Mwanawe Isak’ aliyemfurahia: kipeo cha furaha ya uzee wake, matumaini yake yote ya dunia, kafara atakayotoa kwa Bwanake.
4
Katika njia ya mlima wa Moriya mtoto akamsaili baba yake: “Tazama moto uko, kuni ziko pia, kondoo mume kwa kafara yuko wapi?” Na Ibrahimu akajibu kwa imani isiyoona shaka wala kudhania: “Kondoo mume kwa kafara ya shukrani, ninasadiki Mungu atajipatia.”
5
Je awezaje Ibrahimu kusahau wakati huo wa uchungu na huzuni, na jinsi akajenga huko madhabahu, na tena akamweka mwana ju’ ya kuni? Akakitwaa kisu amchinje mwana, halafu aliposikia neno tamu: “Usifanyie neno sasa kwa kijana, najua wanipenda sana Ibrahimu!”
6
Akainua macho yake kwa haraka, tazama dume la kondoo, nyuma yake, aliyenaswa pembe zake kwa kichaka! Akamtoa akomboe mwana wake. Na malaika akamwita akasema:”Umenitii nami nitakubariki. Na kwa uzao wako mataifa tena wa’barikiwa kwani umenisadiki”.
7
Machozi yamekuwa mengi tangu hapo; wakristo wamekamilika kwa jaribu. Na mlimani mwa Moriya wazikapo matumaini yao, pendo na nasibu. Lakini juu ya mlima wa kafara Mwenyezi Mungu abariki watu wake. Awajulisha nguvu zake na ishara, awajaliza Roho ya ahadi yake.