Indirimbo ya 249 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Zamani mjini mwa Yerusalemu waisrael’ waliabudu. Wakristo wa sasa wanakusanyika kuomba, kusifu Mwokozi.
Msifuni, msifuni Mungu wetu, kwani ametutendea mema! Tutamsifu tu aliyetoka ju’, shangilieni Mwokozi mwema!
2
Mwokozi yu nasi, ame’fumbulia uweza wa kutuokoa. Na yu mwaminifu, atusikiliza, apenda kutupa baraka.
3
Twaomba baraka na mvua ya mbingu kuithibitisha Injili! Wagonjwa wapone, vipofu waone, Tupate ‘batizo wa Roho!