Indirimbo ya 253 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Siku ya furaha inatufikia, siku nzuri katika nchi. Mungu asifiwa mbali na karibu! Malaika wanamshukuru Bwana.
2
Huko Bethlehemu alipozaliwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, pendo la Mwenyezi likadhihirika; raha ya mbinguni imefika kwetu!
3
Ni karama kubwa tuliyoipewa kwa mkono wa Baba Mungu. Roho mfariji anatuongoza, atuonya njia iendayo kwake.