Indirimbo ya 254 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ roho yangu, sikiliza vema, wimbo wa juu unatufikia! Shangwe na raha unatuletea, amezaliwa Mkombozi wetu.
Ahimidiwe Mungu wa mbingu! Na duniani iwe raha na amani!
2
Ninafurahi kwani wimbo huo tungali tunausikia huku. Na kwa upendo Mungu aita: “Mfike kwangu, nitawapa raha!”
3
Katika nchi, mbali na karibu, sauti ya Mwokozi inavuma. Watu wa dhambi wanakuja kwake, awapokea na awaokoa.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 254 mu Nyimbo za wokovu