Indirimbo ya 26 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nakuhitaji, Yesu, Mwokozi wangu mwema, sauti yako nzuri iniletee raha!
Nakuhitaji, Yesu, usiku na mchana! Katika sala yangu unibariki sasa!
2
Nakuhitaji, Yesu, unionyeshe njia! Na unitimizie ahadi za neema!
3
Nakuhitaji, Yesu, uwe karibu nami, nipate kulishinda jaribu la shetani!
4
Nakuhitaji, Yesu, katika mambo yote, kwa kuwa bila wewe maisha hayafai.
5
Nakuhitaji, Yesu, njiani huku chini, nipate kuwa kwako milele na milele!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 26 mu Nyimbo za wokovu