Indirimbo ya 262 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Kitambo bado-vita itaisha, kitambo, na dhoruba zitapoa. Na tena nitalaza kichwa changu mbavuni mwake anayenipenda.
:/: Nitaziona raha na amani, mbinguni hazitakuwapo dhambi.:/:
:/: Nitaziona raha na amani, mbinguni hazitakuwapo dhambi.:/:
2
Kitambo bado- roho yaumizwa, kitambo katika usiku huku. Machozi nina’toka mara nyingi sababu sijaona bado Yesu.
:/: Lakini asubuhi ya milele huko mbinguni sitalia tena.:/:
:/: Lakini asubuhi ya milele huko mbinguni sitalia tena.:/:
3
Kitambo bado ya kuchoka huku, kitambo, tena nitaona Yesu. Na huru mbali na hatari zote nitastarehe mikononi mwake.
:/: Uvuli wote utaondolewa kwa nuru huko kamilifu kweli.:/:
:/: Uvuli wote utaondolewa kwa nuru huko kamilifu kweli.:/:
4
Mateso yangu hayadhuru tena, nitasahau yote kwa Yesu. Nikisumbuka mda duniani, mbinguni sitaona shida, kufa.
:/: Na Mungu atafuta kila chozi, ataondoa maumivu yote.:/:
:/: Na Mungu atafuta kila chozi, ataondoa maumivu yote.:/: