Indirimbo ya 263 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Enyi kundi lake Mungu, muda haba mhimili! Kati’ nchi ya milele mtaona raha tele.
:/: Muda haba, muda haba, tena vita itakwisha.:/:
:/: Muda haba, muda haba, tena vita itakwisha.:/:
2
Usilogwe na dunia, usiache Mungu wako! Katika mabaya, mema ufuate Bwana Yesu.
:/: Siku zote, siku zote! Hivyo utashinda vyote.:/:
:/: Siku zote, siku zote! Hivyo utashinda vyote.:/:
3
Ukichoka safarini, ukiona njia ndefu na hatari za jangwani, Mungu akuburudisha.
:/: Raha huko, raha huko yatuliza msafiri.:/:
:/: Raha huko, raha huko yatuliza msafiri.:/:
4
Kwa imani tunaona nchi yetu ya ahadi. Ni habari nzuri sana: Majaribu yatakoma.
:/: Mbio sana, mbio sana huko ju’ tutaonana.:/:
:/: Mbio sana, mbio sana huko ju’ tutaonana.:/:
5
Tukiitwa na mauti kwa furaha tutahama. Tulivyovitumaini, ng’ambo huko tutaona.
:/: Heri tele, heri tele: ‘ona raha ya milele!:/:
:/: Heri tele, heri tele: ‘ona raha ya milele!:/: