Indirimbo ya 264 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
E’ msafiri jangwani, tazama juu mbinguni! Hapo utaona nyota za faraja na tumaini.
Huko hutayaona machozi wala shida. Mungu atatuliza msafiri mbinguni kwake.
2
Ukisumbuka gizani katika pepo, dhoruba, bado wakati mfupi, nuru itatokea tena.
3
Ukililia wapendwa waliokutangulia, utakutana na wote, hutalia machozi tena.
4
Na karibu na Bwana Yesu utastarehe daima, hutakumbuka mbinguni shida, kufa na sikitiko.