Indirimbo ya 269 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Katika bonde na milima, kwa mataifa mahali pote, peleka neno la wokovu! Msifu Yesu sana!
Msifu Bwana, msifu Bwana! Na tangazeni neno lake, ‘sifuni Yesu daima!
2
Mapema na jioni pia hubiri neno la Bwana Yesu! Tangaza njia ya wokovu, msifu Yesu sana!
3
Lo! Paradiso malaika wanahimidi Mwokozi wetu. Tuimbe nasi sifa yake, tu’sifu yesu sana!
4
Usiyeona kufa bado, uipokee neema leo! Ujisafishe kati’ damu, msifu Yesu Kristo!