Indirimbo ya 284 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Usimtafute Yesu kati’ wafu kaburini! Yu mzima, tumsifu, hakushindwa na kuzimu!
:/: Yesu hai, Yesu hai, mshindaji wa mauti!:/:
:/: Yesu hai, Yesu hai, mshindaji wa mauti!:/:
2
Maadui walifunga Bwana Yesu kaburini, Mungu alimfufua Mwana wake. Furahini!
:/: Yesu hai, Yesu hai, imba hivyo duniani!:/:
:/: Yesu hai, Yesu hai, imba hivyo duniani!:/:
3
Yesu hai, ni habari ya kupasha pande zote. Yu Mwokozi wetu kweli, alitufilia sote.
:/: Yesu hai, Yesu hai, Mkombozi asifiwe!:/:
:/: Yesu hai, Yesu hai, Mkombozi asifiwe!:/: