Indirimbo ya 291 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Mimi mwenye hatia nilikombolewa, Mwokozi alipojitoa. Dhambi zangu na zako alizichukua, kwa damu aliniokoa.
Dhambi zimetundikwa msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.
2
Yesu mwenye upole na mwenye upendo ananitakasa rohoni. Nimepata uhuru kwa Yesu Mwokozi, alikufa msalabani.
3
Namwambata Mwokozi, sitaki kumwacha, kwa kuwa alinifilia. Nakusifu, e’ Yesu, unayenipenda, daima nakushangilia.