Indirimbo ya 294 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya hapo kale!:/: Uwashe moto wako ndani yetu, tusiwe watu wa uvuguvugu!:/:
2
Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya siku ile.:/: Mtume Petro alipohubiri katika nyumba yake Kornelio!:/:
3
Utume Roho yako juu yetu, utupe nasi Pentekoste yetu!:/: Maelfu wenye dhambi waokoke, na neno lako lienee pote!:/:
4
Utume Roho yako juu yetu! Mikono yako uinyoshe sasa,:/: ishara za ajabu zifanyike, wagonjwa uwaponye kati yetu!:/:
5
Uwaamshe waliosinzia, waliochoka huku safarini!:/: E’ Bwana utujie kama kale ulivyowabariki watu wako!:/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 294 mu Nyimbo za wokovu