Indirimbo ya 304 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sifa, uwezo na heshima, kwake Yesu Mwana kondoo. Sifa, uwezo na heshima, ni Mfalme wetu.
Sifa, sifa, mwimbie kwa shangwe Sifa, sifa, Mwana Kondoo.
2
Siku ya kuja kututwaa, tutakwenda kumlaki. Na tena tutamfanana, sifa Mwana Kondoo.
3
Nitafurahi kuondoka nchi hii ya mateso. Nitamkuta Bwana wangu, na Mwokozi wangu.
4
Ninamwimbia tu kidogo, hapa chini duniani, nitamwimbia mara nyingi, huko kwake mbingu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 304 mu Nyimbo za wokovu