Indirimbo ya 318 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nimeliona pendo kubwa mno, na pendo hilo nalifurahia. Na jina lake mwenye kunipenda, Ni Mungu Baba tena Yesu Mwana.:/: Upendo wako nausifu sana, ewe Mungu nawe Yesu Kristo.:/:
2
Mimi mtoto mdogo mbele yako, nakuhitaji unisaidie. Kwa kila kazi na kwa hali zote, kwa majaribu katika dunia.:/: Usiniache mimi peke yangu, uwe nami kwa safari yangu.:/:
3
Nikikuomba uje kwangu Yesu, ukija tena ninaona hofu. Utanishika mimi mwanadamu, sitendi vema mimi mwenye shaka.:/: Nilipendalo silitendi tena, ninafanya nisilolipenda.:/:
4
Nilipokuwa mtoto mchanga, na niliwaza mambo ya utoto. Na kwa wakati wakuwa mzima, nilibadili mambo ya utoto.:/: Matumaini na imani yangu, inakwamilishwa kwa injili.:/:
5
Nimeliona pendo la Mwokozi, aliyenikomboa kati damu. Na damu hiyo si damu ya nyama, ni damu yake Bwana Yesu Kristo.:/: Ee! Mwenye haki kwa wasio haki, umetoa maisha na pendo.:/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 318 mu Nyimbo za wokovu