Indirimbo ya 343 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Bwana Mungu, nashangaa kabisa. Nikifikiri jinsi ulivyo Nyota ngurumo vitu vyote pia viumbwavyo kwa uwezo wako.
Roho yangu naikuimbie jinsi wewe ulivyo mkuu:/:
2
Nikitembea pote duniani ndege uimba na wasikia. Milima upendeza macho sana, upepo nao nafurahia.
3
Yesu Mwokozi utakapo rudi Kulichukuwa kanisa lako. Nitaimba sifa sako milele wote waone jinsi ulivyo.