Indirimbo ya 356 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Sitasahau nilipootoka Yesu aliingiamo rohoni. Mto wa sifa na shangwe watoka, Kisima kile ninacho rohoni.
:/: Ajabu kuu:/: Neema gani napata wokovu.:/: Ajabu kuu:/: Mimi wa dhambi napata wokovu.
2
Katika watu wa dhambi ma elfu, Anichagua Rafiki mpenzi. Mimi ni huru ninamuimbia, wimbo wa roho, zaburi na tenzi.
3
Msalabani Alinifilia, mwili na roho zipate wokovu. Ni pendo gani na neema pia, Anajitoa kwa watu wa dhambi.
4
Roho wa Mungu alinishukia, na kunijaza upendo mkuu. Moyoni mwangu ninashangilia, Ananijaza kwa nguvu ya Yesu