Indirimbo ya 36 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Yesu ameniokoa, amenipa utulivu. Kwake ninaona raha, ninataka kumsifu.
Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini. Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.
2
Kwa furaha ninaimba wimbo mpya wa wokovu. Nisichoke kamwe hapa kumwimbia Mkombozi.
3
Ni habari za neema zakupasha pande zote. Mhubiri, enda mbio kufikia nchi zote!
4
Yesu, siku nita’kufa na maisha ni tayari, ‘nichukue kwako juu penye raha ya milele!