Indirimbo ya 42 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Bwana Yesu amevunja minyororo ya maovu, nimewekwa huru kweli mbali na makosa yangu.
Haleluya, haleluya! Yesu Kristo ni Mwokozi! Haleluya, haleluya! Yesu alinikomboa.
2
Nilipoungama dhambi, nikawekwa huru kweli. Moyo wangu unawaka kwa upendo ‘takatifu.
3
Kamba zilizonifunga zimetoka, nafurahi. Dhambi zilizo ‘sumbua zimetupwa mbali sana.
4
Ninataka kuhubiri: Nimewekwa huru kweli. Nipeleke kwa furaha neno zuri la Mwokozi.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 42 mu Nyimbo za wokovu