Indirimbo ya 47 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nikiona udhaifu na imani haba, nikijaribiwa sana, Yesu anilinda.
Anilinda vema, anilinda vema, kwani Yesu anipenda, anilinda vema.
2
Peke yangu sitaweza kuambata yeye, pendo langu ni dhaifu; Yesu anilinda.
3
Mimi mali yake sasa, alinikomboa, alitoa damu yake; Yesu anilinda.
4
Haniachi kupotea, anilinda sana. Kila ‘mwaminiye kweli, Yesu amlinda



Uri kuririmba: Indirimbo ya 47 mu Nyimbo za wokovu