Indirimbo ya 51 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Naona amani Golgotha alipojitoa Mwokozi,
:/:Na huko nina kimbilio kwa Yesu aliyejitoa.:/:

2
Sitaki ‘tamani fahari na dhambi katika dunia,
:/: Sababu wokovu ninao katika ‘jeraha ya Yesu.:/:

3
Aliziondoa kabisa mizigo na kamba ya dhambi.
:/: Na niliokoka halisi kwa neno la Mungu wa ‘hai.:/:

4
Maneno ya Mungu ni kwetu chakula na dawa ya roho,
:/: na nguvu ya kusaidia mkristo katika safari.:/:

5
Mimi sasa hekalu la Roho, anayemiliki moyoni;
:/: na Yesu ataniongoza kwa njia ya ahadi zake.:/:

6
Uliye dhambini ufike kwa Yesu Mwokozi wa wote!
:/: Anakunyoshea mikono ya pendo kukusaidia.:/: