1
Ni heri kuonga ndugu njiani pa kwenda mbingu. Tukinyong’onyea sana kwa kuwa tu peke yetu, kushirikiana kwa ndugu kunaturudisha moyo, na Mungu atupa nguvu tukiyainua macho.
2
Twafungamana rohoni, tulio wa nyumba yake, huoni ulimwenguni kushirikiana kwetu. Na tuna Mwokokozi mmoja, imani ni moja pia, watoto wa baba ‘moja twashika sheria yake.
3
Furaha ya ulimwengu haitatuvuta tena, Twaona kung’aa kwake ni bure na bila kisa. Lakini tukikusanyika kwa jina la Mungu Baba, atuandalia kweli karamu ilio bora.
4
Tukivumilia hata ukomo wa mashindano, mbinguni tutawaona wakristo wapenzi wote. Hatutatawanyika huko, tu wote umoja kweli, milele tuta’pokaa nyumbani kwa Baba yetu.