Indirimbo ya 89 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Najua jina moja zuri, lapita kila jina huku, lanipa raha na amani, na jina hilo Yesu.
Yesu, jina zuri mno! Yesu, unapenda wote, Yesu, tunalindwa vema katika jina lako.
2
Napenda jina hilo jema, linanivuta kwake Mungu. Na katika huzuni yangu lanifariji sana.
3
Siwezi mimi kueleza uzuri wake jina hili, lakini namwimbia Yesu, nasifu jina lake.