Indirimbo ya 9 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Naiamini damu yako na msalaba wako, Yesu, Mwokozi wangu wa pekee, napata yote kwako.
Uliyoyaahidi na’pata kwa imani. Huwezi kuniacha mimi; napata yote kwako.
2
Kwa damu nimetakasika, na mto wa uzima wako waniletea nguvu tele, napata yote kwako.
3
Nafungwa kwa upendo wako, njiani unaniongoza, na katika hatari zote napata nguvu kwako.
4
Ninakupenda, Bwana Yesu, wanisikia niombapo, wanipa jibu la maombi, napata yote kwako.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 9 mu Nyimbo za wokovu