Indirimbo ya 94 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Lo! Nuru inapambazuka, na vivuli vya usiku vyakimbia; unaulizwa: U tayari? Yesu yuaja upesi!
Na kama vile ‘pepo uvumavyo po pote, habari iendavyo ulimwenguni mwote. Ni neno la furaha, matumaini yetu: Yesu yuaja upesi!
2
Vizazi vingi vimefungwa utumwani kwa minyororo migumu; uhuru ni kwa Bwana Yesu, naye yuaja upesi!
3
Na watu wengi waamka, nuru ya injili yafukuza giza. Tutatwaliwa ‘ju mbinguni; Yesu yuaja upesi!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 94 mu Nyimbo za wokovu