Indirimbo ya 99 mu NYIMBO ZA WOKOVU
1
Siku moja nitamwona Bwana Yesu uso wake. Na milele kwa furaha nitaka’ karibu naye.
Nitamtazama Yesu ju’ ya nyota zote pia, huko kwa ukamilifu nitajua nguvu yake.
2
Hapa ninaufahamu kwa sehemu wema wake, huko nitamtazama na kushiba kwa kuona.
3
Shangwe gani kwa Yesu! Shida zote zitaisha, giza haitakuwapo, na huzuni itakoma.
4
Yesu atafika mbio, Lo! Mwenyewe atashuka! Tutanyakuliwa juu ili kumlaki Bwana.