Indirimbo ya 1 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ Yesus, Mshindaji wa Golgotha, twakusifu! Bendera ya mapenzi ni Alama ya Kushinda. Ulichukua dhambi zetu juu ya msalaba wako. Twakuhimidi, Bwana na Mfalme! Haleluya!
2
Twashinda na zaidi ya kushinda kati’ yote. Kwa damu yako, Yesu, na watuinua moyo. Katika vita na ‘jaribu twaipeleka kwa furaha Bendera yako nzuri ya kushinda kati’ vita.
3
Mbinguni Mkombozi ni Mkuu mwenye sifa. Aliondoa dhambi kwa kutufilia wote. Mwana Kondoo wake Mungu, Umestahili kupokea Uweza, Utukufu na Heshima. Haleluya!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 1 mu Nyimbo za wokovu