Indirimbo ya 3 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Kisima safi sana chatoka msalaba, Kimetufungukia, chasafisha vema. Twaweza kusikia sauti yake Yesu: “Unifuate sasa kwa kiti cha neema”.
Kisima cha msalaba, damu ya Yesu Kristo, chatusafisha sisi sote na dhambi na uchafu.
2
Ufike, mwenye dhambi, kisima ni karibu. Uache dhambi zako, upumzike hapa! Katika damu yake kabisa utapona, Tazama msalaba, kisima kitokako!
3
Kisima hicho safi cha damu ya Mwokozi. Kinatutia afya na nguvu ya kushinda. Mfalme wetu, Yesu, tumhimidi tena! Furaha yetu yote ni kushukuru Mungu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 3 mu Nyimbo za wokovu